Village elders call for uniforms, stipend from government

By Timothy Mugo

Wazee wa Mtaa kaunti ya Migori wameiomba serikali kuu kuwapa sare za kuvalia wakiwa kazini pamoja na malipo kiasi ya kujikimu katika maisha.

Akiongea katika eneo la Oruba, jimbo la Suna magharibi katika kaunti ya Migori, bwana Kennedy Oketch ambaye ni mzee wa mtaa alisema serikali inastahili kuwapatia sare ambayo ingetumika kuwatambulisha kwa urahisi kwa wananchi na kuwawezesha kuwatumikia kwa urahisi.

Bwana Oketch alisema kuwa sare hizo zingetumika kuashiria mamlaka ya ofisi hiyo ya mzee wa mtaa.

Oketch pia alisema wazee wengi walioteuliwa wadhfa huo waliishi kwa maisha ya ufukara na hivyo aliiomba serikali kuwazawadia malipo kama shukrani kwa kazi zao.

Alisema zawadi hiyo ingewapa motisha katika kazi zao.

Aidha alisema kuwa ukosefu wa malipo ulipelekea baadhi yao kujihusisha katika vitendo vya ugaidi na kusema kuwa malipo hayo yangewapa motisha kazini.

Wazee wa mitaa huteuliwa na kusaidiana na machifu na manaibu wa chifu katika maangalizi ya usalama katika mitaa .