VIDEO: Bodaboda riders threaten not to pay taxes over bad roads at Posta – Nyasare – Apida in Migori town

Part of a road barricaded by demonstrators in anti IEBC protests

Na Ripota Wetu
Waendeshaji wa boda boda wameandamana mjini Migori wakilalamikia barabara mbovu na miundo msingi mjini Migori na viungani mwake huku wakiapa kutolipa ushuru kwa kaunti ya Migori.

Wakiongozwa na Hillary Ogaro,waendeshaji hao wa bodaboda na wakaazi wa maeneo ya Nyasare,Apida,Magina na Nyikendo waliandamana na  kuwafurusha maafisa wa kusanya ushuru wa kaunti ya Migori .

Waandamanaji hao waliisuta serikali ya kaunti ya Migori kupitia kwa mwakilishi wa wodi ya Suna ya kati wakitaka barabara za maeneo hayo kutengenezwa.

Haya yanajiri juma moja baada ya wakaazi wa eneo la posta na Aroso kulalamikia barabara mbovu katika eneo hilo lililoko kwenye wodi hiyo mjini Migori.

WATCH VIDEO HERE: